Roomy Jones Amuandikia Diamond Barua ya Wazi "Inatosha Kusaidia Vipaji Mtaani Hao Hao Uliowasaidia Wako Busy Kukuharibia"

 


Ameandika @romyjons kupitia ukurasa wake wa Instagram. "Barua ya wazi kwa mdogo wangu nasibu abdul ama @diamondplatnumz


Nakumbuka ulivyoanza kutoa nyimbo na wasanii tofauti na wa nchi tofauti. Soko lako hadi number zako zilikua kwa kasi sana kwenye mziki wako hadi kupelekea kua msanii bora afrika mashariki. Sio sababu wewe ndio ulikua unajua kuimba peke ako hapana!!


Bali ulikubali kuwekeza muda,akili hadi pesa kwenye biashara yako hadi ikafika kipindi tukawa tunashangaa kolabo zako. Mara na davido mara p square mara mr flava na ndio watu waliokua wa moto kweli kweli kipindi hicho!!!


Ushauri wa wazi kwako!! Hata kama ni biashara ama kukuza vipaji vya mtaani nadhani sasa inatosha. Kwanini usiwekeze nguvu, akili, pesa kwenye biashara yako ya radio na tv?


Wanasema “kikulacho kinguoni mwako” Walewale uliowafungulia njia ndio wapo nyuma yako kukukashifu, kukuponda hata kukukebehi!!


Tukiangalia top charts wasanii wote ni wale waliotoka kwako ama waliopo kwako. Hii ni wazi kwamba usingekua na wasanii number za mwanzo zote huenda zingekua za kwako kwa kipindi kirefu mno. Ni kweli kila anaekua ana hitaji kutoka kwenye familia na kujitaftia ugali mwenyewe na kutengeneza familia yake.


Sasa ni lazima kumponda ama kumkebehi mzazi wako?


Lil wayne bado yupo na kina drake na juzi waliperform pamoja kwenye tamasha la drake. Usher raymond bado yupo na justin beiber na anaendelea kunufaika na matunda yake. Sijajua huku kwetu ni ulimbukeni wa pesa nyingi za ghafla,tabia ama uelewa ni mdogo!!


Jaribu kuwekeza nguvu zako kwako mwenyewe tuone kwa sasa hivi huenda ungekua na album moja na chris brown sasa hivi. Kuliko kuwekeza nguvu,muda kwa watu wasio na shukran!!!!


Naomba kuwasilisha !!!! From your lovely brother 🖤🖤🖤" - unasomeka ujumbe huo wa Romy Jons.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad