Saido Arejea Tena Tanzania




KLABU ya Geita Gold imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Mrundi, Said Ntibazonkiza kwa mkataba wa miaka miwili ikiwa ni miezi mitatu tangu nyota huyo alipotemwa na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Mei 30 mwaka huu.
KLABU ya Geita Gold imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Mrundi, Saido Ntibazonkiza kwa mkataba wa miaka miwili ikiwa ni miezi mitatu tangu nyota huyo alipotemwa na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Mei 30 mwaka huu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ililiambia Mwanaspoti, Saido amekamilisha taratibu zote na viongozi wa timu hiyo na muda wowote kuanzia sasa atatua nchini.

"Ni kweli tumefikia makubaliano hayo baada ya mapendekezo ya benchi letu la ufundi, ni mchezaji mzuri ambaye licha tu ya umri wake ila tunaamini atatusaidia sana kwenye michuano mbalimbali hususani ile ya Kimataifa," kilisema chanzo hicho.

Mwanaspoti linatambua nyota huyo aliongea na viongozi ili kumtumia tiketi ya ndege ila ilishindikana hivyo kukubaliana kutumia gari akitokea kwao Burundi kisha maofisa mbalimbali wataenda hadi mpakani kumpokea kisha kujiunga na timu hiyo.

Nyota huyo alijiunga na Yanga Oktoba 12, 2020 akitokea Klabu ya Vital’O ya nchini kwao huku akiwahi pia kuzitumikia timu mbalimbali za Kaysar Kyzylorda, Akhisar Belediye, SM Caen na Kysar.

Akiwa na Yanga msimu uliopita alihusika kwenye mabao 10 katika Ligi Kuu Bara akifunga saba na kuchangia matatu (assisti) kwenye michezo 18 aliyocheza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad