Samia ateua 22 kuwa majaji, yumo mwanaye kigogo Chadema



RAIS Samia Suluhu Hassan ameteua maofisa ishirini na wawili (22) kuwa Majaji wa Mahakama Kuu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 6 Agosti, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu,  Zuhura Yunus imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza Agosti 4,2022.

Katika orodha hiyo yumo Happiness Ndesamburo ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa Chadema (2000-2015), Philemon Ndesamburo.

Wengine ni walioteuliwa; Kevin David Mhina, kabla ya uteuzi huu Bwana Mhina alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani;


 
Gabriel Pascal Malata, kabla ya uteuzi huu ,Gabriel alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali;

Adrian Philbert Kilimi, kabla ya uteuzi huu, Adrian alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;

Happiness Philemon Ndesamburo, kabla ya uteuzi huu, Happiness alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;


Victoria Mlonganile Nongwa, kabla ya uteuzi huu, Victoria alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;

Obadia Festo Bwegoge, kabla ya uteuzi huu, Obadia alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;

Ruth Betwel Massam, kabla ya uteuzi huu, Ruth alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;

Godfrey Ntemi Isaya, kabla ya uteuzi huu, Godfrey alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;


 
Gladys Nancy Barthy kabla ya uteuzi huu, Gladys alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;

Haji Suleiman Haji, kabla ya uteuzi huu, Haji alikuwa Mwendesha Mashitaka Mfawidhi Mahakama Kuu, Zanzibar;

Fatma Rashid Khalfan, kabla ya uteuzi huu, Fatma alikuwa Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora;

Abubakar A. Mrisha, kabla ya uteuzi huu, Abubakar alikuwa Wakili wa Serikali;


Lusungu Hemed Hongoli, kabla ya uteuzi huu Lusungu alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;

Monica Peter Otaru, kabla ya uteuzi huu, Monica alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;

Kamana Stanley Kamana, kabla ya uteuzi huu Bwana Kamana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi (TAMISEMI);

Hamidu Rajabu Mwanga, kabla ya uteuzi huu Bwana Hamidu alikuwa Mkurugenzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi;

Marlin Leonce Komba, kabla ya uteuzi huu, Marlin alikuwa Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi;


 
Dk. Mwajuma Kadilu Juma, kabla ya uteuzi huu Dkt. Mwajuma alikuwa Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Mzumbe;

Dk. Cleophas K.K. Morris, kabla ya uteuzi huu Dk. Cleophace alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu Dar es Salaam;

Asina A. Omari, kabla ya uteuzi huu Bi. Asina alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC);

Aisha Zumo Bade, kabla ya uteuzi huu, Aisha alikuwa Wakili wa Kujitegemea na

Mussa Kassim Pomo, kabla ya uteuzi huu, Mussa alikuwa Wakili wa Kujitegemea. Tarehe ya uapisho wa Majaji Wateule itatangazwa baadaye.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad