Serikali "Hakuna Mgonjwa wa Homa ya Nyani Tanzania"


 Serikali kupitia Wizara ya afya imesema kuwa Mpaka sasa, hakuna mgonjwa aliyetambulika na kuthibitika kuwa na ugonjwa wa homa ya nyani (Monkeypox) hapa nchini.


Kauli hiyo imebainishwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe leo Mkoani Manyara, wakati akitoa taarfa kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Nyani (MonkeyPox) ambapo hivi karibuni, Shirika la afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwepo kwa ugonjwa huo katika baadhi ya nchi Duniani.


Amesema Ugonjwa huo unaoambukizwa na virusi vya Monkeypox, na dalili za ugonjwa huo mara nyingi huonekana kuanzia wastani wa siku 5 hadi 21 tangu mtu apate maambukizi.


“Hivyo ni vyema wananchi wakaondoa hofu maana Serikali kupitia Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaendelea kufuatilia hali ya ugonjwa huu katika nchi unakotokea.”Amesema Dkt. Sichalwe.


Sambamba na hilo Dkt. Sichalwe amesema madhara ya ugonjwa huo ni pamoja na kifo (case fatality rate), huku akiondoa hofu kuwa, madhara ya kifo sio makubwa na kusema wakiugua wagonjwa 100, watatu hadi sita ndiyo wanaweza kufariki na mara nyingi ugonjwa hupona wenyewe.


“Wizara imeandaa mipango ndani ya masaa 72, na mpango wa muda mrefu wa kukabiliana na ugonjwa huu kama utatokea, Wizara imeandaa mwongozo wa matibabu ambapo utatumika iwapo tukipata mgonjwa.” Amesema mesema Dkt. Sichalwe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad