Shaffih Dauda Awashukia Simba "Siku Chache Zimesalia Kuelekea Simba Day na Hawana Jezi Mpya Alafu Tunalazimishwa Kuiita Club Kubwa..Excuse Me"


Kuna dunia ambayo Simba wanaishi, ni dunia ambayo wanaamini hakuna makosa, wanaamini ni wakubwa, wanaamini kila kitu kinachofanyika ni sahihi sana

Hata pale ambapo wameharibu watahitaji kupamba na kuonekana hawajaharibu, hata pale watapopaswa kuambiwa maneno machungu ya ukweli watahitaji nyimbo za mapambio

Siku chache zimesalia kuelekea Ngao ya Jamii hawana jezi mpya, masaa yamesalia kuelekea Simba Day hawana jezi mpya, lakini ndio klabu hii ambayo tunalazimishana kuiita kubwa, klabu yenye weledi? Excuse me

CEO kama Mtendaji wa klabu you are in for this, suala la jezi sio option ni lazima, suala la merchandise ni compulsory na linafahamika, inatia ukakasi kwa namna mnavyoyaendea mambo, inafikirisha sana

DIGALA siwezi kukubali kuwa kwenye dunia ya praise and worship, sio dunia nzuri ya kuficha makosa na kuonekana mema, sio dunia nzuri mambo yakienda mrama watu wasake namna ya kujificha sio sawa na hii ni AIBU

Kwa Shabiki wa Simba anayejua mpira na kuelewa maana ya biashara anafahamu kuwa hili mmeharibu, lakini kwa Shabiki yule oya oya tu ataona DIGALA nachonga, ataona Digala ana nongwa ila in details nawapa dawa ya kuwaponya

Kwakuwa hili mmeshaharibu sio vyema msimu wa 2023/24 mkarudia tena makosa, hakuna excuse kwa matukio ambayo yana time frame, hakuna excuse ya Mdhamini wala usafiri, jezi sio suala la bahati mbaya

Hakuna wimbo wa maana utakaotungwa kuepusha aibu hii, hakuna wimbo utatungwa kuepusha kadhia hii, ndio ni klabu maarufu sasa pambaneni kuusaka UKUBWA, ukubwa una details zake, ukubwa una indicators zake, BADILIKENI

DIGALA naamini mpira ni darasa kubwa, utawala ni darasa kubwa, muda wa kuendelea kujifunza upo na naamini tukae darasani kama Wanafunzi watiifu na sio Walimu wakorofi

DIGALA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad