Shaffih Dauda Awashukia Tena Simba "Ukubwa Uko Wapi Kama Mmetoa Jezi Chache Mmetesa Watu Sana Leo"


Jezi ni huduma kwa Mashabiki na ni biashara kwa timu na Mtengenezaji, ila changamoto ya Simba mfano leo ni kama mnawapa jezi bure ikiwa hii ni huduma tena kubwa

Kila siku nawaambia UKUBWA sio maneno ni process na ni merit sio favor jana tu nimetoka kusema hichi kitu na leo kimetokea, Mashabiki wengi wameumizwa sana hawajapenda hichi mlichofanya

Mmetoa jezi ngapi? Ni chache ambazo hazikidhi mahitaji ya hata 50% ya mashabiki, wameteseka sana Mashabiki kisa kuhitaji huduma ya timu yao? Wametoka watu Mbagala, Kibaha na karibu kila sehemu kwenda Sinza pekee?

Ukubwa upo wapi kama hatuwapi thamani hawa mashabiki, nilitarajia kuona mnaomba radhi, simply ni kuomba radhi wala hakuna kingine

Mfano Yanga wametoa jezi 100,000 na wakatangaza kila sehemu ambayp zinapatikana jezi, tunavozungumza zimefika nchi nzima kwakuwa waliweka utaratibu tena mzuri mno

Kama mmeshindwa basi igeni hata kwa Yanga, ombeni namna wawambie wamewezaje kufanikisha bila kelele yoyote

Ombeni radhi Mashabiki

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad