Vikosi vya usalama vya Somalia vimethibitisha vifo vya zaidi ya watu 10, katika shambulio la wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu kwenye Hoteli moja katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.
Kulingana na maafisa hao wa Usalama, wamesema watu wenye silaha walilipua vilipuzi nje ya Hoteli ya Hayat mjini Mogadishu, kabla ya kuingia na kuwafyatulia risasi raia, ambapo hata hivyo baadhi ya wafanyakazi na wageni wakiwemo watoto waliokolewa na kitengo maalum.
Mashuhuda katika tukio la shambulizi lililosababisha mauaji ya watu zaidi ya 10 katika Hotel ya Afrik jijini Mogadishu nchini Somalia. Picha na EPA.
Kenya: Mwananchi awasilisha pingamizi uapisho wa Ruto
Milipuko mikubwa na milio ya risasi imeendelea kusikika alfajiri ya hii leo Agosti 20, 2022 kuashiria maafisa wa polisi na wanamgambo walikuwa bado wanaendelea kupigana ili kupata ukombozi wa maeneo yaliyovamiwa na waasi hao.
Kundi lenye uhusiano na Al-Qaida la Al-Shabaab, lilidai kuhusika na shambulio hilo kwenye tovuti inayounga mkono Shabaab na Hayat inaelezwa kuwa eneo maarufu kwa maafisa wa serikali ambao kundi hilo la kigaidi limekuwa likipambana nalo kwa miaka 15 katika shambulio hilo kubwa zaidi katika mji mkuu tangu rais mpya wa Somalia kuchaguliwa Mei, 2022.