Simba SC yaachana na Hassan Dilunga

 




Hatimaye Uongozi wa Simba SC umefunguka kuhusu Kiungo Mshambuliaji Hassan Dilunga, ambaye hakuonekana katika utambulisho wa Wachezaji wakati wa Tamasha wa Simba Day jana Jumatatu (Agosti 08).


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu hiyo Ahmed Ally amesema Dilunga amemaliza mkataba wake na Simba SC, hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi chao kwa msimu ujao, ambao utaanza rasmi mwishoni mwa juma hili.


Amesema Kiungo huyo aliyeitumikia Simba SC kwa miaka mitano iliyopita, alimaliza mkataba wake tangu mwishoni mwa msimu uliopita 2021/22, ambapo kikosi chao kilimaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nyuma ya Mabingwa Young Africans.


Amesema sababu kubwa ya kufanya hivyo ni baada ya kuthibitika Dilunga atakua nje ya Uwanja kwa muda mrefu kutokana na Majereha aliyoyapata msimu uliopita, hivyo Simba SC imeona ni bora kumuacha ili aendelee kujiuguza.


Hata hivyo Ahmed amesisitiza Uongozi wa Simba SC utaendelea kuwa karibu na Dilunga katika kipindi hiki ya kujiuguza, kwani alipata madhila hayo akiwa katika majukumu ya klabu hiyo ya Msimbazi.


“Hassan Dilunga amemaliza Mkataba wake ndani ya Simba na hivi sasa ni majeruhi kwa hiyo hatukuuongezea naye Mkataba Mpya na hata tungemuongeza ana muda mwingi wa kukaa nje kwa ajili ya kujiuguza ila tutamsapoti kama Klabu Lakini si sehemu ya mipango ya Simba sc kwajili ya msimu 2022/23” amesema Ahmed Ally

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad