Simba yaipiga bao Yanga



TUMEUJAZA!  ndivyo wanavyosema  mashabiki wa Simba  baada ya kufanya kufuru kwenye tamasha lao la Simba Day ambalo kilele chake ni leo Agosti 8.

Licha ya idadi ya mashabiki wa Simba kuwa kubwa nje tayari uwanja umejazwa huku vaibu la tamasha likiendelea kupamba moto kutokana na burudani zinazoendelea.

Ni wazi mashabiki wa Simba wameipiga bao Yanga ambao licha ya kuwa wengi walishindwa kuujaza uwanja.

Ngoma kali na ustadi wa Dj Joozey vinaonekana kuwakosha mashabiki wa Simba waliopo kwa Mkapa.


 
Kwa wingi huu ni wazi kuwa muda wowote milango ya uwanja huu inaweza kufungwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad