Singida Big Stars Yakanusha Mbrazil wao Kuchukulia na Yanga


KATIKA kuhakikisha imedhamiria kutetea mataji yake kuelekea msimu mpya wa 2023/23, Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji jana iliunda Kamati Maalum ya Mashindano yenye watu wanane, ikiongozwa na Rodgers Gumbo.

Taarifa iliyotolewa jana mchana na klabu hiyo imewataja wajumbe wanaounda kamati hiyo kuwa ni Mustapha Himba, Lucas Mashauri, Seif Ahmed 'Magari', Pelegrinus Rutayuga, Davis Mosha na Majid Suleiman 'Kaburu'.

Wakati huo huo, klabu ya Singida Big Star imekanusha tetesi zinazoenea kwa kasi kwenye mtandao ya kijamii tangu jana kuwa ina mpango wa kubadilishana winga wao raia wa Brazil, Derio Federico na klabu ya Yanga kwa kuwapa Jesus Moloko.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Singida United, Dismas Ten, amesema hakuna mazungumzo yoyote ya kuuza mchezaji au mabadilishano na klabu yoyote.

"Ninachoweza kusema Derio ni mchezaji wa Singida Big Stars na hivi sasa ninavyokuambia yuko mazoezini na kikosi chake baada ya mechi dhidi ya Mtibwa, tuna mkataba naye wa miaka mitatu na hakuna jambo lolote lililofanyika kuhusu mchezaji huyo kwa sababu huu ni mwanzo tu wa mkataba wake," alisema Ten.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad