Siku mbili nyuma msanii tokea Record Label ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuchu ameweka record ya kuwa msanii wa kwanza wa kike tokea ukanda wa chini ya jangwa la Sahara kuwa na subscribers wengi kwenye mtandao wa YouTube baada ya kufikisha Subscribers milioni 2.1 na kumpiku Mnigeria Yemi Alade aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo kwa kuwa na Sub milioni 2 kamili.
Hii imekuwa ni jambo jema kwa muziki wa Tanzania, ambapo kwenye list ya Wasanii kumi wa kike wenye subscribers wengi kusini mwa Jangwa la Sahara, tuna wasanii wawili, Nandy akiwemo pia. Jambo baya ni kuona subscribers wa Zuchu wanamfanya Diamond aonekane yuko sahihi kwenye mikataba dhidi ya wasanii wake, wengi wamekuwa na comments zinazo onyesha kuwa hata msanii akitozwa milioni 800 ya kuvunja mkataba hapaswi kulalamika.
Kuna kitu inabidi ifahamike, Subscribers is just the number na sio pesa, mtu kaweka record ndio, ila unaweza kuta Tiwa Savage ambaye ana 1.1M subscribers account yake inaingiza mtonyo mrefu zaidi kuliko account ya Zuchu, kwanza payment ya YouTube ina vipaumbele vyake na inavary nchi na nchi, kuna vitu vinaitwa CPM, CPC na RPM inabidi uvijue ndio unaweza elewa pesa ya YouTube ikoje.
Hakuna msanii anayetaka kuvunja mkataba kama anafaidika nao pia, hivyo tusiwe wepesi wa kujudge vitu ikiwa hatuwezi kuviwaza kiundani. Hasa Sijui tunashangilia record Au pesa inayoingia kupitia hao subscribers? ambayo pia inaenda kwenye label.
Bongo bana😁
By Sajomedia