Tanasha: Jimbo Liko Wazi, Nipo Tayari Kuwa na Mwanaume Mwingine




MWIMBAJI na mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Tanasha Donna ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpenzi.

Tanasha ambaye ni mzazi mwenzake na Diamond Platnumz amesema kuwa yuko tayari kumpa mwanaume mwingine nafasi katika moyo wake.

“Nipo single! Labda kuna mtu ambaye anaweza kuwa mpenzi anayefuata, inaweza kuwa,” amesema Tanasha.


Tanasha Donna ni Mama wa mtoto mmoja aliyezaa na Staa wa Muziki Barani Afrika kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz
Mama huyo wa mtoto mmoja alibainisha kuwa hazingatii sura ya mwanaume wala utajiri wake anapotafuta mchumba.


 
Alifichua kuwa jambo la msingi analozingatia kwa mwanamume anayekusudia kuchumbiana naye ni tabia yake.


Tanasha ni Membo na Mwanamitindo kutoka nchini Kenya
“Tabia ni muhimu sana kwangu. Ni ufunguo wa kila kitu maishani kwa sasa kando na Mungu, mimi ni muumini pia,” alisema.

Tanasha pia alidokeza kuwa mwanaume anayetazamia kuchumbiana naye ni sharti awe mwenye bidii na mcha Mungu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad