Siku ya leo klabu ya Simba umetambulisha jezi zake na mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa na mwitikio mkubwa juu ya kununua jezi za klabu yao.
Akiongea na Bongofive Mtangazaji wa mpira wa Azam Ramadhani Ngoda ameeleza kuwa kwa namna vilabu vya Tanzania vinavyotambulisha jezi zao vitavifikia vilabu vikubwa duniani akivitaja kama Real Madrid na Manchester United.
Mbali na hilo ameeleza namna ligi kuu msimu huu wa 2022/23 utakavyokuwa mgumu akivitolea mfano vilabu vilivyojipanga vizuri kama Singida Big Stars, Namungo na Dodoma Jiji.