Michuano ya Kombe la Dunia 2022 inatarajia kuanza siku moja mapema baada ya FIFA kukubali kuwaruhusu wenyeji Qatar kuanza kwa mechi dhidi ya Equador.
Kabla ya mabadiliko hayo mechi ya kwanza ilitakiwa kuchezwa Novemba 21 kati ya Senegal na Holland, mechi ya pili ilipangwa kuwa kati ya England na Iran huku wenyeji Qatar wakipangwa kucheza mechi ya tatu dhidi ya Equador.
Qatar wameomba kufungua dimba la michuano hiyo na hivyo FIFA kukubali na sasa mechi yao itachezwa Jumapili Novemba 20 ambayo ni siku ya ufunguzi.
Mabadiliko haya yataisogeza mechi kati ya Senegal na Holland kuwa mechi ya 3 huku mechi ya pili ikibaki kama ilivyopangwa hapo awali.
Kabla ya kuanza kwa mechi hiyo kutakuwepo na shughuli ya ufunguzi rasmi wa kombe la dunia 2022.