Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewataka wadau kupuuza taarifa potofu zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuhusu mialiko ya Mkutano Mkuu wa Mpira wa Miguu Afrika (CAF) uliofanyika Arusha Tanzania.
Kwa mujibu wa TFF “Mkutano wa 44 uliofanyika Jijini Arusha Uliandaliwa na CAF wenyewe TFF walikuwa wenyeji Tu.”
“Wajumbe wa Mkutano wametajwa katika Katiba ya CAF na waalikwa wengine huwalikwa na CAF na sio TFF kama inavyopotoshwa.”
“Nafasi ya TFF ilikuwa ni kutafuta Mgeni rasmi wa kufungua Mkutano huo na sio vinginevyo.”
“Ukiondoa Kamati ya Ndani ya Maandalizi (Loco) washiriki wengine wote walialikwa na CAF yenyewe.”