TFF yavunja benchi la Ufundi Taifa Stars




Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limefikia makubaliano ya kumuondoa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars Mdenmark Kim Poulsen pamoja na benchi lote la Ufundi la Taifa Stars. huku kocha Kim atasalia kwenye timu za vijana mpaka mkataba wake utakapomalizika .

Kocha Mkuu wa klabu ya Namungo FC Mzambia Hanour Janza ametangazwa na TFF kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars na atasaidiwa na kocha msaidizi Mecky Mexime huku kocha wa Magolikipa atakuwa ni Juma Kaseja.

TFF imefanya mabadiliko hayo ya benchi la ufundi ikiwa ni siku moja tu imepita tangu kikosi cha timu ya taifa Taifa Stars kipoteze mchezo wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya wachezaji wanaocheza Ligi za ndani CHAN dhidi ya timu ya taifa ya Uganda kwa kichapo cha bao 1-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad