Twaha Kiduku "Nitapambana Kwa ajili ya Watanzania"

 


Bondia Twaha Kassim ‘Kiduku’ ameanza Kambi ya kujiandaa na Pambano la Kimataifa ambalo huenda likaunguruma Septemba 24, katika mkoa ambao utatangazwa baadae.


Kiduku ambaye kwa mara ya mwisho alionekana ulingoni mwanzoni mwa mwaka huu akipambana na Alex Kabangu kutoka DR Congo, amedhamiria kuendelea kuonyesha moto kwa wapinzani hususan wanaotoka nje ya nchi.


Akizungumza kutoka mkoani Morogoro Kiduku amesema ameingia Kambini mwishoni mwa juma lililopita akiwa na matumaini kufanya vizuri.


Amesema dhamira yake ni kuhakikisha aneendelea kuwafurahisha watanzania ambao kila siku wamekua wakimfuatilia anapokua ulingoni.


“Nitapambana na mpinzni kutoka nje ya nchi, muda ukifika atatangazwa hadharani na Promota, mashabiki wangu hawatakiwi kuwa na presha kabisa, nipo kwa ajili yao.”


“Ninajiandaa kwa ajili yao, sitawaangusha kwa sababu nimekua nikiwapa ladha ya ushindi kila ninapopata nafasi ya kupanda ulingoni, najua thamani ya Bendera ya taifa langu, nitapambana kwa ajili ya watanzania wote.” amesema Kiduku

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad