Ujumbe wa Marekani Kukutana na Uhuru, Ruto na Raila jijini Nairobi

 


Ujumbe kutoka nchini Marekani unatarajiwa kukutana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, naibu wake William Ruto (Rais mteule) na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

Ujumbe huo unaongozwa na Seneta wa Delaware Chris Coons uliwasili nchini usiku wa Jumatano ulipokelewa na Balozi wa Marekani Meg Whitman.

Ujumbe huo uko katika ziara rasmi katika nchi tano za Afrika.

"Ni jambo la kustaajabisha kukaribisha ujumbe unaoongozwa na Seneta Chris Coons, ni kituo cha tatu katika ziara ya nchi tano barani Afrika!

Ujumbehuo utakutana na wahifadhi wa mazingira, watoa huduma za afya na mashirika yanayofanya kazi kuwawezesha wasichana," Whitman aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Haya yanajiri siku chache baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) Wafula Chebukati, kumtangaza William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022.

Ujumbe huo pamoja na mambo mengine utajadili masuala ya malengo ya pamoja, ikiwa ni pamoja na afya, usalama na ustawi wa kiuchumi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad