Ukishangaa ya Pogba Basi Hujasikia Haya ya Adebayor Ambapo Ndugu zake Walitaka Awalipe Mishahara


Wakati tunashangaa sakata la Paul Pogba na Ndugu yake Mathias, tusisahau sakata la Emmanuel Adebayor pia na familia yake, Jamaa alisimulia mengi mpaka kutaka kujiuwa mara kibao.

Adebayor aliwahi kulaumiwa hakumsaidia Kaka yake mpaka amefariki lakini anasema alipopewa taarifa za kuuguwa kwa Kaka yake alisafiri mpaka Togo ili kumjulia hali Kaka yake.

Kwa mshangao mkubwa sana alipofika Mama yake alimwambia huwezi kumwona kwasasa ila atoe pesa na wao watahudumia, Adebayor aliwapa pesa nyingi sana japo baadae walipinga.

Kama hivyo haitoshi Adebayor alisimulia kisa cha Dada yake ambaye alimwambia anataka nyumba ya Pauni 1.2 Million nchini Ghana na Ade alimtumia hizo pesa ila ajabu aliporejea Afrika na kutaka kwenda kuiona nyumba akagundua ameipangisha na hakai yeye.

Mbaya zaidi alimnunulia hiyo nyumba ili Dada yao huyo aishi na mdogo wao ila ajabu alimtumja hadi mdogo wake ili apangishe, Adebayor alipohoji alitukanwa sana kwenye simu na Dada yake.

Kwa kumalizia Adebayor aliwahi kuwekewa kikao na Ndugu zake wakitaka amjengee kila mmoja nyumba na awalipe mshahara kila mwisho wa mwezi kwakuwa yeye ana pesa.

Baadhi tu ya mambo ambayo Adebayor alipitia na naona stori nyingine kwa Paul Pogba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad