Vanessa Mdee Awalipua Kampuni ya Ziiki Media "Naombeni Mnilipe Pesa Zangu"


Supastaa @vanessamdee leo Alhamisi ameamka na mood ya kukusanya madeni yake, kupitia ukurasa wake wa twitter asubuhi hii ameitolea uvivu kampuni ya MZIIKI ambayo imekuwa ikifanya distribution kwa wanamuziki mbalimbali kwa kile alichoeleza kwamba anaidai kampuni hiyo pesa zake.

Vanessa ameeleza kwamba amejaribu kutumia njia nzuri kudai pesa hizo lakini imefikia hatua kampuni hiyo kumkalia kimya.

“Tafadhali @mziiki nawaomba mnilipe pesa zangu kwa makubaliano tulionayo. Nimejaribu the professional way na team yangu sasa imefikia hatua ya nyie kutokujibu, ameandika Vanessa Mdee kupitia ukurasa wake wa twitter.

Ikumbukwe, hii sio mara ya kwanza kwa Vanessa kuichana kampuni ambayo anayoidai, miezi kadhaa iliyopita amewahi kuichana Benki moja jina kapuni akidai immalizie pesa zake kufuatia alikuwa Balozi wa Benki hiyo. Hata hivyo, haijajulikana kama Benki hiyo ilishamlipa maana @vanessamdee hakusema tena.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad