Vipers yamjaza upepo Sure Boy




KIUNGO wa Yanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amefichua kuwa kufungwa na Vipers kwenye mchezo wao wa kirafiki hakujawanyong’onyeza ila ndio kwanza kumewaongeza nguvu za kupambana na kuwaita mashabiki kushuhudia ubora wao.

Yanga itakuwa mwenyeji kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa ligi dhidi ya wapinzani wao Simba ambao wanaingia kusaka kisasi baada ya msimu uliopita kukubali kichapo cha bao 1-0 lililofungwa na Fiston Mayele.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sure Boy alisema hawana hofu yoyote kuelekea mchezo huo kutokana na ubora wa kikosi walichonacho huku akiweka wazi kuwa muda utaamua nani bora kati yao na Simba.

“Tuna kikosi bora na cha ushindani maandalizi yanakwenda vizuri kila mchezaji mejindaa kuhakikisha anashinda mechi ya Jumamosi ili kuendeleza pale tulipoishia. Kupotez dhidi ya Vipers kumeongeza chachu ya ushindani, twendeni mashabiki tutawafurahisha,” alisema na kuongeza:


“Kitu kikubwa nadhani kila mtu anaelewa ukubwa na presha ya mchezo wa dabi inavyokuwa kwa sababu kila upande umekuwa ukitafuta matokeo ili kuwa katika nafasi nzuri kwenye ushindani na mshindi kwenye mchezo huo ni bingwa, hakuna asiyetaka taji la Ngao tukutane”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad