Wasanii Wakazi na ROMA Mkatoliki Wararuana Mtandaoni Kisa Album ya Stamina


Wakali wa muziki wa Hip Hop Bongo, rappa Roma Mkatoliki pamoja na rappa Wakazi wamejikuta kwenye mjadala ulioweza kuleta mabishano baada ya Roma kuibua mjadala huo katika mtandao wa Twitter akimueleza Wakazi ana kitu cha kujifunza kupitia kwa Stamina kulingana na idadi kubwa ya streams za album yake katika mtandao wa Boomplay ambayo haina hata miezi 6 tangu itoke huku album ya Wakazi ikiwa na miaka 4 na haijafikisha kiwango kikubwa cha streams.


"Kaka Yangu Wakazi, Kisimani Album ina miaka 4 lakini ina 15.2K streams na kuna manyimbo kama 18. Huyu mdogo wako Stamina album haina hata miezi 6 ana 6.5M streams na ana nyimbo 13 tu. Hiyo ni Boomplay sijaenda Youtube bado. Kuna cha kujifunza hapa Kaka.. Unajua ni kwa kiasi gani nakupenda." - Inasomeka Tweet ya Roma.


Rappa Wakazi aliijibu Tweet hiyo akimueleza Roma kwamba, hana album, hajawahi kwenda Big Brother Afrika na hawezi kwenda. Na kudai Roma ana wivu wengine wakifanikiwa. Anajiona analijua game kuliko Wote, Ametweet Wakazi akimjibu Roma.


Aidha akiendelea na majibu yake, Wakazi amemtaka Roma awaulize Boomplay album yake ya "Kisimani" wameipata lini na kwa nini.


Sogeza picha kushoto..


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad