Watu 19 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne ikiwemo trekta



Watu 19 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne ikiwemo trekta Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.


Ajali hiyo imetokea usiku wa August 08, katika Barabara ya Isaka kijiji cha Mwakata ambapo imehusisha gari dogo aina ya IST namba ya usajili T 880 DUE, Hiace T 350 BDX, Lori T 658 DUW pamoja na trekta.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Kamanda wa Polisi Geita ACP. Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa ajali na kusema Dereva wa trekta amekimbia na juhudi za kumsaka zinaendelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad