Wema Sepetu Avuja Ukimya Video yake ya Kimahaba na Whozu




Wema avuja ukimya video yake ya kimahaba na Whozu Wema avuja ukimya video yake ya kimahaba na Whozu

Saa chache baada ya video yake akiwa kimahaba na Rapa Whozu, msanii wa sinema za Kibongo Wema Sepetu, ameibuka na kuzungumzia video hiyo.

Kipande hicho cha video kinachomuonesha Wema akijibebisha kwa Whozu kimevuja mapema Agosti 30, 2022 ambapo miongoni mwa watu wa kwanza kukisambaza alikuwa ni mtangazaji mbeya maarufu, Maimartha Jesse.

Baada ya Maimartha kuposti video hiyo na maoni kuwa mengi, Wema aliibuka kwenye uwanja wa komenti na kuandika hivi:

“Hivi kwanini lakini mnapenda kuni attack na rafiki zangu... So watu wakiwa washkaji sana ni wapenzi...? Msiwe hivyo bwana....” aliandikia Wema na kusindikiza na emoji za kuziba sura kama vile anaona aibu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad