Yanga Kweli byuti byuti, Mashabiki Wajitokeza



Klabu ya soka ya Yanga leo Agosti 6 2022 inaadhimisha kilele cha wiki ya mwananchi huku ikiwa na kauli mbiu ya Byuti Byuti na wamelithibisha hilo kutokana na wingi wa mashabiki waliojitokeza uwanjani na burudani iliyotolewa kutoka kwa wasanii mbalimbali. Anaripoti Damas Ndelema…….(endelea)

Tamasha hilo linalofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ambalo huwa ni rasmi kwa ajili ya kutambulisha benchi la ufundi pamoja wachezaji watakao itumikia timu hiyo katika msimu mpya wa ligi kuu ya NBC na kutoa fursa kwa mashabiki na wapenzi wa klabu kupata fursa ya kuona wachezaji wake kabla ya msimu mpya kuanza ambao tayari ratiba yake ishatoka


Pia mashabiki wameweza kuitikia wito na kujitokeza kwa wingi katika kilele hicho cha na kupata burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii na kuitekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya klabu yao ambao ni byuti byuti

Aidha bado burudani zinaendelea na kutakua na mechi za timu ya wanawake’Yanga queens’ , timu ya vijana chini ya mika ishirini pamoja na timu ya wakubwa ambayo itacheza na mabigwa wa Uganda Vipers Fc ambao watacheza majira ya saa1 jioni na kukamilisha kilele hicho cha wiki ya mwananchi.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad