MSANII wa Bongo Fleva, Zuchu ametoa experience yake ya shoo ambayo aliwahi kuogopa zaidi katika maisha yake ya muziki ambayo ameitaja kuwa ni shoo ya #IamZuchu launching aliyofanya katika Ukumbi wa Mlimani City wakati akitambulishwa rasmi na lebo yake ya #WCBWasafi.
Zuchu amefunguka hayo kupitia kipindi cha The Switch cha wasafi FM; “Siku ya kwanza nilikua naenda kuperform #iamzuchu launching watu walikuwa wanapitia kipindi cha Corona, kwa hiyo ya kwanza tulifanya indoor hakukuwa na watu, so ya pili ile siku sikulala.
“Napenda jinsi Boss alivyoichukulia ‘mbona unaenda pale unaua nakuamini’ na pia sikufanya mazoezi sana nilifanya siku moja tu kesho yake ndio shughuli yenyewe.
Zuchu
“Pia, usiku huohuo ilikuwa ni lazima tumalizie wimbo wa #Mauzauza nilio mshirikisha mama yangu (Khadija Kopa) ili EP ikitoka na huo wimbo uwepo ndani.
“So, kulikuwa na vitu vingi vinatokea kwa pamoja nakumbuka nilikua studio, Boss ananikazania nimalize wimbo na nilikua naogopa kumwambia nimechoka, kwa hiyo alivyotoka nikaanza kulia.
Kina #Mbosso wakaanza kunibembeleza, nilikua nimechoka pamoja na uoga na nilikuwa naharisha siku nzima nilikua naogopa sana nikawa nawaza vipi kesho nikaperform Watanzania wasinikubali?
“Kwa hiyo ndio shoo ambayo sitakuja kuisahau kwenye maisha yangu, nafikiri ile shoo ilinipa uoga ambao sijawahi kuupata tangu nimeanza muziki,” amesema Zuchu.