Afya ya Mfalme Charles III Yaanza Kuzua Utata, Madaktari Watoa Ufafanuzi


WAKATI Mfalme Charles akitawazwa kurithi kiti cha ufalme Jumamosi ya Septemba 11, 2022 baada ya kifo cha Malkia Elizabeth, gumzo kubwa limeibuka kufuatia kusambaa kwa picha kwenye mitandao ya kijamii, zikionesha vidole vya mikono ya Mfalme Charles vikiwa amevimba vidole vya mikono yake.


Kusambaa kwa picha hiyo, kukawaibua madaktari na wataalamu wa afya, akiwemo Dokta Gareth Nye kutoka Chuo Kikuu cha Chester ambaye ametoa maoni yake wakati akihojiwa na Gazeti la Daily Star kuhusu hali hiyo ya Mfalme Charles III.


Katika mahojiano hayo, Dokta Gareth amesema vidole kuvimba na kuwa vyekundu, ni dalili ya magonjwa mbalimbali, ukiwemo ugonjwa wa Oedema ambao husababisha majimaji ndani ya mwili kujaa kwenye viungio vya mikono na miguu.


Dokta Gareth akaongeza kuwa, pia hiyo inaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa Arthritis ambao huwakumbwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 ambao nao husababisha sehemu mbalimbali katika mwili kuvimba, ikiwemo vidole vya mikono na miguu.

Mfalme Charles III amerithi kiti cha ufalme akiwa na umri wa miaka 73 ambao kwa mujibu wa Dokta Gareth, ni umri ambao binadamu hukumbwa na magonjwa mengi kutokana na uzee.

Hata hivyo, Dokta Gareth amesema hawezi kuwa na hitimisho la moja kwa moja la nini kinachomsumbua Mfalme Charles na kueleza kuwa wanaoweza kutoa majibu yanayoeleweka ni madaktari wake.

Daktari mwingine, Rinky Kapoor ameibuka na kueleza kuwa huenda Mfalme Charles akawa anasumbuliwa na ugonjwa wa Oedema ambao pia huwaathiri zaidi watu wenye umri mkubwa, hususan kuanzia miaka 65 na kuendelea.

“Dalili za nje za mgonjwa wa Oedema zinazoweza kuonekana kwa macho, ni pamoja na kuvimba vidole vya mikono, kuvimba miguu na endapo ukibonyeza eneo lililovimba, hubonyea na kuchelewa kurudi katika hali yake ya kawaida,” amenukuliwa Dokta Kapoor.

Ameeleza kwamba, dalili nyingine ya Oedema, ni ngozi kuvutika na kung’ara huku wakati mwingine ikibadilika na kuwa nyekundu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad