Aliyedaiwa kufa akazikwa, aibukia nyumbani akiwa mzima





Familia moja katika kijiji cha Gatwikira nchini Kenya imechanganyikiwa baada ya ndugu yao aliyesadikiwa kufa na kuzikwa kurudi akiwa mzima.

Joseph Kiarie (35) aliondoka nyumbani mwezi Juni kwenda kufanya kazi Nairobi na mwezi mmoja baadae alipoteza mawasiliano.

Familia yake inayoishi katika Kaunti ya Muranga ilipewa taarifa kuwa mtu anayefanana na Kiarie ameuawa na mwili wake umehifadhiwa.

Familia ilifuatilia,ikautambua mwili na japokuwa baadhi yao walikataa kuwa yule siye ndugu yao, mwisho walimzika.

Miezi miwili baadaye kijana huyo alimpigia simu mama yake na sasa amerudi nyumbani. Familia inangojea uamuzi wa Mahakama ili iweze kuufukua mwili waliouzika ili uweze kurudishwa unakotakiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad