Aliyesimamishwa kazi kwa agizo la Shaka asema ataendelea na majukumu yake




Tabora. Mrajisi wa vyama vya ushirika, Dk Berson Ndiyege ametekeleza maagizo yaliyotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsimamisha kazi mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Tabora, Absalom Cheliga.

Kigogo huyo amesimamishwa kazi jana Ijumaa  Agosti 19, 2022 muda mchache baada ya katibu wa Itikadi na Uenezi wa  CCM, Shaka Hamdu Shaka kutoa maagizo ya kumsimamisha kazi kutokana na tuhuma za kushindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Cheliga amesema taarifa za kusimamishwa kazi  hajazipata kutoka kwa mkuu wake na kwamba  ataendelea na majukumu yake ya kazi.

"Mimi nimesikia kwenye vyombo vya habari kuwa  nimesimamishwa kazi lakini bado sijapata taarifa rasmi kutoka kwa bosi wangu, kwa hiyo naingia ofisini kama kawaida," amesema Chelinga.


Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Dk Ndiyege,  Cheliga anasimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

”Amesimamishwa kazi kwa mujibu wa kanuni namba  37 ya kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Akiwa katika wilayani Uyui kwenye ziara yake mkoani Tabora kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, Shaka aliomba serikali kumuondoa mrajisi huyo baada ya kupata malalamiko kila wilaya juu ya utendaji wake kazi.


“Changamoto za bwana huyu imekuwa donda sugu , tumetoka Kaliua analalamikiiwa, tumetoka Sikonge analalamikiwa, tumetoka Urambo analalamikiwa, leo tuko Uyui watu wanalia na huyu bwana. Urasimu umekuwa mkubwa sana."

“Utitiri na ukiritimba umekuwa mkubwa  kiasi kwamba  unadumaza jitihada na huko tunakotoka hajasajili vyama kwa sababu kuna mawakala wanapita chini kwa chini. Mbunge  kasema na mimi taarifa ninazo, wapo mawakala wanapita chini kwa chini kuwaambia wakulima  nenda kajiunge pale. Yeye sio  kazi yake, yeye sio jukumu lake la nani akajiunge ushirika gani," amesema

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad