1: WHAT A MATCH .. WOW. JUST WOW👏 Quality. Quality. Quality. Dakika 90 zenye hadhi ya kuitwa Derby! YANGA UNBEATEN MECHI 40 za Ligi.
2: Refa Ahmed Arajiga katikati ya Stori kubwa ya mchezo. Bajana alistahili kadi nyekundu, hakutoa. Dube alichezewa rafu [Haikuwa ndanj ya boksi], akapeta .. Krosi ya Lomalisa mpira ilitoka wote nje, akamezea.. Morrison alimkanyaga Lusajo kwa kudhamiria! Refa mkubwa aliyefanya makosa makubwa kwenye mchezo mkubwa!
3: Benchi la Ufundi la Azam FC lilikuwa na mpango mzuri dhidi ya Yanga. Dakika 45 walifanya Build Up kwenye ‘Tempo’ ya chini na wakawa na haraka ya shambulizi walipofika kwenye ‘Penetration phase’. Kwanini walifanikiwa?
4: Katikati walikuwa na Issa Ndala, Mzuri kwenye Build Up.. mbele yake akawa Sospeter Bajana, mzuri kama Box To Box.. mstari wa ulinzi wa Yanga kwenye kiungo kulikuwa na Aucho na Bigirimana.. Wakaadhibiwa na changamoto ya Kasi. ‘Back 4’ ya Yanga ikawa inafikika kirahisi sana.
5: Kipindi cha Pili, Nabi katika Ubora wake wa siku zote.. Akaja na ‘Sub’ mbili za akili sana.. Feisal na Djuma Shabani.. Feisal akaongeza kasi katikati. Djuma akaja kuipa nguvu safu ya ushambuliaji. Hatua zake zikamruhusu Aziz Ki kudumbukia ndani kwenye eneo la mwisho
6: FEISAL WAKISHUA🙌 What A Player! Tofauti ya Feitoto na wengine ni Uwezo wa kudumbukia eneo sahihi katika wakati sahihi.. Silaha yake ya kupiga kwenye Target, ni jambo ambalo hakuna kipa angependa kukutana nayo
7: ALI AHAMADA👏 Kipa mzuri sana.. Yes kuna makosa kidogo kwenye bao la pili la Feisal Lakini he was Brilliant👏 Achana na save yake ya penalti, uwezo wake wa kucheza zile krosi na kuwa na mchango kwenye build up
8: Sospeter Bajana.. From Hero to Zero! Game aliiweka kwenye himaya yake mwanzoni Lakini baadae presha ikamzidi, akatoka mchezoni kabisa
9: Kipre Jr👏 What A Kid! Dogo anajua sana. Kasi yake imeacha maswali mengi sana kwa Lomalisa. Kitu pekee cha kuboresha ni ‘maamuzi ya mwisho tu
10: Yanga inamuhitaji Yanick Bangala kama Kiungo, sio Beki. Nafikiri ‘Sub’ ya Sure Boy ilitakiwa kuwahi haraka pia.. Well Done NDALA👍
Nb: Refa ni Mwakinyo mwenye Filimbi 😀