Askari watatu wafutwa kazi Arusha




JESHI la Polisi mkoani Arusha limewafukuza kazi askari wake watatu kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi hilo ikiwemo ukosefu wa nidhamu kazini, huku likiwatahadharisha wengine wenye tabia kama hizo kuziacha.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Justine Masejo.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Justine Masejo, wakati akizungumzo na chombo kimoja cha habari ofisini kwake.

Kamanda Masejo amesema askari hao kwa nyakati tofauti wamebainika kwenda kinyume na maadili ya kazi ya Jeshi la Polisi ikiwemo kushindwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utendaji kazi.

"Hao askari tumewaondoa katika Jeshi letu na tutaendelea kufuatilia na wengine watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na kiapo walichokikubali wakati wanajiunga na Jeshi hilo,”

"Niwatake askari wengine wenye tabia kama hizo kama wanataka kuendelea na kazi ya kulitumikia jeshi la polisi basi wahakikishe wanafuata nidhamu na maadili ya kazi," amesema Kamanda Masejo.

Hata hivyo, Kamanda huyo amesema kwa sasa hawezi kuwaweka wazi waliofukuzwa kwani bado upelelezi unaendelea wa kuwachunguza askari wengine na wataendelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wale watakaobainika kuvunja sheria za nchi basi watawafikisha katika mikono husika.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad