Askofu wa Kanisa la Anglikana Dodoma Afariki Dunia Baada ya Kuongoza Ibada ya Mazishi


Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa Jijini Dodoma, Kapteni, George Chiteto amefariki dunia muda mfupi baada ya kutoa mahubiri katika ibada ya mazishi ya mke wa Askofu mwenzake, Hilda Lugendo iliyofanyika wilayani Muheza mkoaniTanga.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dkt. Maimbo Mndolwa aliyeongoza misa hiyo katika Kanisa la Kristo Mfalme Muheza, amesema taarifa waliyopewa
kutoka hospitali ni kuwa Askofu huyo alipatwa na mshtuko wa moyo.

"Madaktari wametuarifu kuna kitu kinaitwa cardiac arrest, alikuwa na shida ya pressure (shinikizo la moyo) na kisukari,"

"Yeye alikuwa mhubiri na kwa kweli mahubiri yake yaliwavuta watu na neno lake la mwisho ni (mlango umeandaliwa twendeni)," amesema Askofu Mndolwa.

Akifafanua jinsi kifo cha askofu huyo kilivyotokea, msemaji wa kanisa hilo, Maiko Luoga amesema, Askofu Chiteto alihubiri katika misa hiyo na kumaliza, kisha alipokaa alishiwa nguvu na kukimbizwa katika hospitali tule ya Muheza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad