Barakah the Prince ni Funzo Kwa New Generation Mnapokuwa Kwenye Peak, Mkishuka Kila Mtu Mchawi


Jeuri itakufanya usifiwe kwa muda mchache, maana ukingo wa tabia hiyo hauko mbali, Epuka sana Ngozi ya mwili ifanane na tabia yako, na hata kama ni kufanana basi ngozi iwe ang'avu. Kuna wasanii wanaofanya vizuri hivi sasa, kama Dayoo, Marioo, Lody Music ,Lony Bway n.k , Kipindi hiki mnacho fanya vizuri, izingatieni nidhamu yenu na kuifikiria zaidi kesho yenu, maana Leo mnayoiishi hivi sasa iliwahi kuwa ni leo ya mastaa wengi ambao kwa sasa wanaishi kesho yao, hapa kuna mawili, either Uishi mtaa wa Gofu au wa Bao, na tunaona Wasanii wengi ambao hawakuifikiria kesho yao wana utajiri mkubwa wa lawama hii leo kuliko makaratasi ya ATM, si lazima uwe na kikubwa, bali uwe na kinacho weza kuyamudu maisha yako ambacho kinajengwa na leo yako. Mfano mzuri kwenye safari ya muziki wenu anaweza kuwa Baraka.


Nasikitika kuona msanii kama @barakahtheprince_ ambaye nidhamu ya kipumbavu imezamisha nafasi yake kwenye muziki, ambapo kwasasa hajui nani amtupie lawama kwenye maisha yake ya sanaa, Alimpaka sana Alikiba kipindi anatoka Rock star, akimsifu vilivyo Diamond, Diamond sio chizi, aliona kama ameweza kumtukana Alikiba hadharani , basi ipo siku atakuja kumtukana na yeye, akamkalia mbali, siku hazigandi, hivi karibuni Barakah aliandika walaka mrefu akiwatuhumu Diamond na Mama yake kwa uchawi.


Kijana wa hovyo akiperform mbele ya watu watatu na bia za bei chee kichwani kwenye show moja usiku wa kuamkia leo huko Mwanza, ameona @officialalikiba ndio kiki yake ya kurudia mjini. Anaongea maneno hata leo akijisikiliza mwenyewe alivyo kuwa akiongea,atajionea aibu. Yote haya yanatokana na stress za muziki, akikumbuka miaka minne iliyopita alikuwa kwenye peak, Leo ni kama hayupo, Lazima imuumize akili.


Kipaji bila ni dhamu, ni ujinga usio na faida kwenye unacho kifanya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad