Breaking News: Polisi Yaua Panya Road Sita, Walikuwa Wakienda Kufanya Uhalifu


JESHI la Polisi Kanda maalum Dar es Salaam, limefanikiwa kuwaua Waalifu sita maarufu kama Panya Road waliokuwa wakielekea eneo la Goba kufanya uhalifu jana Septemba 17,2022.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu, Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum, Jumanne Muliro

Ambapo amesema baada ya taarifa fiche kutoka kwa Wananchi wema, walibaini kuwa, waalifu hao wakiwa Kwenye Noah, kutoka eneo la Mabibo kuelekea Goba kufanya uhalifu, na ndipo walipowakamatia eneo la Makongo Area 4.

"Tuliweka mtego, na tuliwasimamisha eneo la Makongo, na walikuwemo watuhumiwa 9,


Watuhumiwa wa ujambazi wakiwa na vifaa vya jadi maarufu panya Road, walitoka na mapanga ndani ya Noah hiyo kwa lengo la kutoroka chini ya Ulinzi,"alisema.

na kuongeza:

"Askari waliwatadharisha na kujihami, na kupiga risasi juu, na kutaka Kila njia wasitoroke, lakini katika purukushani hizo Sita walijeruhiwa vibaya na watatu wakatoroka,

Waalifu hao sita, walipeleka hospital lakini wakapoteza maisha, "alisema.


Kamanda Jumanne Muliro alisema eneo la tukio waliweza kukamata mapanga Tisa, na kisu kimoja na dhana za kuvunjia katika matukio mbalimbali.

..Uchunguzi wa awali, kwa watuhumiwa hao umebaini kuwa miongoni ni viongozi wa makundi hayo ya kutumia silaha, na wapo waliopataka kuhukumiwa na kutoka, Kisheria.

Aidha, Kamanda Jumanne Muliro amewataja waliotambulika kati ya waliopoteza maisha kuwa, Salum Juma Maarufu kama Babu Salum umri kati ya miaka (20-27) mkazi wa Mbagala,

Pia mwingine, ni Kharifa kharifa mkazi wa Buguruni ambaye nae inaonesha aliwahi kukamatwa kwa makosa ya uhalifu wa kutumia mapanga Dar es Salaam.

Pia amebainisha katika Upelelezi umebaini kuwa, vinara hao walishiriki kwenye tukio la Kawe, na eneo la Buguruni kwa kuiba na kuua,

Kamanda Jumanne Muliro amesema, Jeshi la Polisi linaendelea kutekeleza kwa haraka agizo lililotolewa na Mkuu wa Jeshi hilo la kuwashughulikia waalifu nchini.

"....Jeshi linawapongesa Wananchi kwa kutoa taarifa za usalama kwa watu wanaopanga ama kutekeleza vitendo vya uhalifu. Jeshi la Polisi linaendelea kuwatahadharisha kuacha mara Moja matukio ya uhalifu, na watakao kahidi wataendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua,

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad