Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Wilaya ya Igunga, Ally Hemed amesema moja kati ya changamoto kubwa iliyojitokeza Wilayani humo kwa baadhi ya maeneo ni Makarani wa Sensa kukutana na vitendo vya kishirikina ambapo walipokuwa wakienda kwenye makazi au nyumba wanakutana na miti au vichaka badala ya kuona makazi halisi.
“Baada ya kuonesha dhahiri jambo hili litaathiri zoezi la Sensa, Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Igunga ambaye ni Mkuu wa Wilaya, Sauda Mtondoo alifunga safari kwenda kuonana na Wazee Wilayani humo na kuelezea kadhia hiyo ndipo wakatoa baraka zao na baadaye Makarani walipokuwa wakienda kufanya kazi hiyo ya Sensa walikuta makazi na kuwakuta Watu halisi badala ya vichaka na miti”
Mkuu huyo wa Wilaya ya Igunga amesema tukio hilo liliwapa somo na kujua umuhimu wa kuonana na Viongozi wa kimila na Wazee kabla ya kufanya chochote.
Kwa upanede wa Wilya ya Tabora Mjini changamoto ilikuwa ni Mtemi wa Jamii inayoishi kwenye Hifadhi ya Igombe iliyopo jirani na Kijiji cha Ikomwa kuzia Watu wake wasikubali kuhesabiwa jambo ambalo Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Chacha alifika kuongea na Mtemi huyo akimueleza umuhimu wa Sensa ambapo alikubali kuwaondoa Watu wake ndani ya Hifadhi ili kusogea Kijiji jirani na wakahesabiwa.