Cleopatra Malkia Anayesadikika Kuwa Mwanamke Mzuri Zaidi Kuwahi Kutokea Duniani




MALKIA Cleopatra ni maarufu zaidi kati ya malkia wote waliowahi kutawala Misri. Cleopatra alizaliwa Alexandria mwaka wa 69 K.K (kabla ya kristo) Wakati wa utawala wa familia ya Ptolemy kwenda kwa Ptolemy XII.

Cleopatra lilitokea kuwa jina maarufu ndani ya familia, kwani mama yake alilipenda kiasi cha kuchukiza kwa wengine lakini pia ndiye alikua binti mkubwa. Cleopatra hakua Mmisri, isipokuwa alikuwa Macedonia familia yake ikitoka katika kipindi cha utawala wa Alexander the Great. Cleopatra alikuwa mtawala wa kwanza katika familia yake ambaye aliongea lugha halisi ya Misri.

Cleopatra mwenye miaka 18 mapema anathibitisha umahiri na uwezo mkuu wa kutawala, hususani katika historia ya kipindi hicho cha Medditerania. Lakini ukaribu wake na utawala wa Roma, baadae unakuja kupoteza uhuru wa Misri.


Malkia Cleopatra
Inasadikika kuwa huyu ndiyo mwanamke mzuri kuliko wote katika historia ya dunia. Ametajwa katika vitabu kadhaa ikiwemo Biblia na aliishi kwa miaka 39. Cleopatra alikuwa ndiyo mtawala wa mwisho wa Kigiriki kutawala Misri na ndiyo aliyekuwa Farao wa Kwanza wa kike mgeni. Alizaliwa mwaka 69 na akiwa na miaka 18 akatawazwa kuwa Malkia.


Cleopatra ni neno la Kigiriki linalomanisha “baba yangu ni maarufu” Cleopatra ni jina walilolopewa mabinti wa kifalme wa kigiriki huku wale wa kiume wa kifalme waliitwa Ptolemy.

Hivyo Cleopatra huyu tunayemzungumzia hapa alikuwa ni Cleopatra wa Saba na wa mwisho. Dola la Misri lilitawaliwa na Ugiriki tangu mwaka 323 baada ya Alexander Mkuu kuishinda Misri na utawala huu uliisha mwaka 30 baada ya Cleopatra kujiua kwa kumruhusu nyoka aina ya Cobra kumgonga kifuani.

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa Mitandao

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad