Dada Aliyenasuliwa Kutoka Mateso ya Saudia Amrukia kwa Hasira Ajenti wake JKIA




Kulikuwa na Hali tete uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta baada ya mwanamke Mkenya ambaye alikuwa ameokolewa kutoka Saudi Arabia kukutana ana kwa ana na wakala wake.

Dada Aliyenasuliwa Kutoka Mateso ya Saudia Amrukia kwa Hasira Ajenti wake JKIA
Mwanamke huyo wa Kenya alishangaa ni kwa nini wakala wake wa usafiri alienda kumwona katika uwanja wa ndege. 

Mwanamke huyo alikuwa ametoka kupokelewa na familia yake na marafiki alipomwona wakala wake kati ya umati mdogo.

Katika video iliyosambaa sana mitandaoni, mwanamke huyo aliyechanganyikiwa alijaribu mara moja kumkabili ajenti huyo wa kike ambaye alimshutumu kwa kumsafirisha hadi taifa la mashariki ya kati, ambako alipitia mateso yasiyoelezeka.


Familia yake ilionekana kujaribu kumzuia mwanamke huyo asikabiliane na wakala huyo, lakini hatimaye alifanya hivyo na akasikika akimuuliza kwa nini alimuuza katika taifa hilo.


"Huna hata haya kuja kuniona hapa? Unapaswa kuwa unasaidia watu! Hiyo ofisi yako uiondoe. Utalipa! Kila kitu ambacho familia yangu ilipoteza utakirudisha!" dada huyo aliwaka.

Alimwaga machozi huku akimrukia wakala aliyetoweka eneo la tukio.

Haya yanajiri siku chache baada ya Wakenya walio ng'ambo kuchangisha KSh 130, 000 ili kumsaidia Diana Chepkemoi aliporejea nchini baada ya kudhulumiwa ughaibuni.

Chepkemoi aliacha masomo katika chuo kikuu cha Meru na kuhamia Saudi Arabia kwa kazi ambayo alitarajia ingemlipia karo.

Kwa bahati mbaya, Chepkemoi aliangukia mikononi mwa mwajiri katili ambaye alimzuilia na kumdhulumu.

Aliokolewa baada ya hadithi yake kusambazwa mitandaoni kwa kasi, na kuwalazimu maafisa wa serikali kuchukua hatua.

Licha ya simulizi zake za kutisha kkutoka kwa mwajiri wake huko Uarabuni, baadhi ya wanawake bado walionekana kwenye uwanja wa ndege, wakielekea nchini humo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad