Habari Njema...Pambano la Ngumi la Mwakinyo na Liam Smith Kurudiwa, Promota Hakuridhika na Maamuzi ya Refa


Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amethibitisha rasmi kuwepo kwa pambano lake la marudiano dhidi ya Liam Smith Januari 23, 2023 hii ni baada ya promota Benjamin Shalom wa pambano lake kutoridhishwa na maamuzi ya refa kwenye pambano hilo lililomalizika kwa utata.


"Kutokana na mchezo wa jana (juzi) na kitendo cha Refa kuwa unfair kwangu kimemlazimu Promoter Benjamin Shalom kutupa nafasi ya re-match na Liam January 23" - ameandika Mwakinyo kupitia ukurasa wake Instagram.


Itakumbukwa, usiku wa Jumamosi, Septemba 3, Mwakinyo alipoteza kwa TKO round ya 4 katika pambano lake lililochezwa jijini Liverpool, Uingereza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad