Baada ya kutangaza kupunguziwa adhabu ya Faini kutoka Milioni 20 hadi Milioni 10 lakini anaendelea na adhabu ya kifungo cha miaka miwili cha kutojihusisha na Soka, aliyekua Msemaji wa Young Africans Haji Manara ameibuka na kuonesha kupuuzwa kilichotangazwa na Kamati ya Rufaa ya TFF.
Manara ameweka andiko la kupuuzia maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya TFF katika Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, akiandika: Alhamdulillah 🙏🏻
Back 2 School Baby Girl 🔥🔥
Alfajiri ya leo nilimsindikiza Bint yangu mkubwa kurejea Istambul Uturuki,ambako anaendelea na masomo yake ya Shahada ya kwanza nchini humo ,,akiwa ktk mwaka wake wa pili wa masomo.
Kwangu hilo ndio muhimu kupita haya mengine ya mapito..hususan yanayojiri kila Usiku Mkubwa.
Watoto wa Maskini Mtaji wao Mkuu ni Elimu,,ndicho kitu tulichoamrishwa kuwekeza kwao ,,Ukiwekeza ktk eneo hilo,kinachobaki ni kumuomba Mungu tu.
Kiuhalisia,Maisha ya Wanetu yanategenea uwekezaji wa kielimu tulioufanya kwao,, Ni Fardhi kusomesha Wanao kwa Imani ya dini yoyote ile..And We have no Choice.
Yes,,Yaliyotangazwa jana na Wafalme juu yangu, ni sehemu ya Changamoto zetu za kidunia na niliyatarajia Pasi na Shaka.
Ndugu zangu,Jamaa,Marafiki na Wananchi wenzangu msifadhaike hata tone na hzi hukumu dhidi yangu,,Haki haijawahi kushindwa milele,,Is the matter of time.
Tuendelee kuwa na Subira Kwa Mungu,
Mungu aliye Mkuu na anaetujua sote Waja wake na tunayoyatenda kwa dhahir na kwa siri.
Once again,,Goodbye Hamida Haji Manara,,Nakupenda Mwanangu 💛❣️
Ubarikiwe katika Kuisaka Elimu 👏