Haji Manara Awajibu TFF "Kununi Hizo Hizo Zilimbadilisha Chikwende Kwa Kahata, Kibu Kucheza Bila Uraia"


Anaandika Msemaji wa Yanga SC, Haji Manara juu ya taarifa ya TFF.

“Hata haieleweki kimejibiwa kitu gani? Na kwa nini Issue ya Yanga uharaka wa kujibu unakuwa mkubwa mno?”

“Kanuni hizi hizi zilizombadilisha Chikwende Kwa Kahata? Kanuni hizi hizi zilizomhalalisha Kibu kucheza bila kupata uraia?”

“Au mnazungumzia zipi ndugu zangu?”

“Kazi yenu na kusaidia Wachezaji wacheze mpira na sio kuwazuia na ndio maana bila baraka zenu ITC ya Kisinda isingepatikana na faini alilipishwa nani?”

“Last season tena kwa maksudi,Yanga pamoja na kuomba kucheza na Washabiki kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa, hamkupeleka barua CAF. Matokeo yake Club ikakosa mapato mengi kwenye mchezo dhidi ya Rivers ya Nigeria, na sio mapato tu, kucheza bila mashabiki nyumbani kunaweza kuchangiwa na kutolewa mapema kwenye Mashindano yale.”

“Wiki hyo hyo wenzetu Team Pendwa walicheza na Washabiki wao.”

“TFF kanuni kuwa favoured ni kwao tu ila Kwa Yanga zinavunjwa?”

“Mbona hamkuwahi kujibu kuhusu kuwanyang'anya Yanga haki ya kucheza bila mashabiki?”

⚽“Naendelea kuwakumbusha,,Yana mwisho haya

#Bugati”


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad