Haki ya Faragha Kwa Wafungwa wa Tanzania Iko Hivi


Serikali imesema suala la haki ya faragha kwa Wafungwa na Wenza wao itaanza kutolewa pale ambapo mifumo ya kisheria na miundombinu ya Magereza itakapokidhi kutolewa kwa haki hiyo ambapo masuala mengine yatakayozingatiwa ni usalama, mila na desturi za Watanzania, kwani haki hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa faragha.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni leo September 13 2022 na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akijibu Swali la Mbunge wa Viti Maalumu Bahati Keneth Ndingo aliyetaka kufahamu lini Serikali itaweka mfumo utakaoruhusu Wafungwa kupata haki ya faragha na Wenza wao.
#

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad