Hamisa Mobetto "Nimeamua Kuishi Maisha Yangu


MOBETO: NIMECHAGUA KUISHI MAISHA YANGU Hamisa Hassan Mobeto@hamisamobetto ; ni mwanimitindo wa kimataifa na msanii wa muziki nchini Tanzania, ambaye anasema kuwa, katika maisha yake amechagua kuishi na siyo kukaa kama wengine wanavyoyachukulia maisha.

Mobeto anasema kuwa, kwa kufanya hivyo ndiyo maana hapati shida yoyote kutoka kwa waja wanaomzunguka kwenye maisha yake.

Akizungumza Mobeto anasema kuwa, anachopenda kwenye maisha yake ni kuishi bila stresi kabisa na ndiyo maana maisha yake yanasonga na madili yanazidi kuongeza kila kukicha kwa sababu moyoni ana furaha tele.

“Nimechagua kuishi maisha yangu mimi na si vinginevyo ndiyo maana kila kukicha sichuji na sichukii hata kidogo, maisha yangu ni mazuri kwa maana nina furaha moyoni mwangu na nina amani siku zote,” anasema Mobeto; mama wa watoto wawili mwenye madili kibao ya ubalozi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad