Hatimaye Uber na Bolt Watangazwa Kurejea Kutoa Huduma za Usafiri Kwa Njia ya Mtandao Tanzania


Hatimaye Uber na Bolt Watangazwa Kurejea Kutoa Huduma za Usafiri Kwa Njia ya Mtandao Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imesema, Kampuni za usafiri kwa njia ya mtandao za Bolt na Uber zinatarajia kurejea kutoa huduma za usafiri nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo ametoa taarifa hiyo akiwa Arusha leo, itakumbukwa Kampuni hizo kwa nyakati tofauti, zilisitisha kutoa huduma za usafiri za magari na kubaki na bodaboda pamoja na bajaji.

Suluo amesema wamesikia kilio cha Kampuni hizo na wameitana kukaa meza moja kwa mazungumzo na tayari wamekubaliana kutatua tatizo ili kurejesha huduma.


"Tuliwaita wakae na Wawakilishi wao wa Afrika, tukaanza September 5- 8, 2022 tumemaliza mazungumzo ambapo kuna taarifa tunataka watuletee kimaandishi ili kutoa maamuzi na leo ndio mwisho wa muda tuliokubaliana na tutatoa maamuzi yatakayowasaidia wote wakiwemo Umoja wa Madereva Taxi (TODA)”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad