Baada ya Majaji wa Mahakama Kuu kumaliza kusikiliza mashauri ya Pingamizi la Matokeo ya Urais pamoja na Utetezi, Septemba 5, 2022 wanaweza kutoa maamuzi yafuatayo:
Iwapo Mahakama itaona dosari kubwa zilizoathiri kwa kiasi kikubwa matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), inaweza kubatilisha Uchaguzi huo na kuagiza kupigwa Kura upya ndani ya siku 60 au kukosoa mchakato wa Uchaguzi na kusema dosari hizo hazistahili kubatilisha Matokeo
Iwapo itabaini kuwa Rais Mteule hakupata 50% pamoja na Kura 1 halali, itaamuru marudio ya Uchaguzi ambayo lazima yafanyike ndani ya siku 30. Na kama haitaona dosari yoyote ya msingi, itaidhinisha ushindi wa William Ruto na kuruhusu kuapishwa rasmi Septemba 13, 2022
Uamuzi wa Mahakama Kuu utaamuliwa kwa wingi wa Kura za Majaji na Mahakama hiyo ndiyo yenye Mamlaka ya juu, iliyoundwa chini ya Katiba ya Kenya ya 2010 ambapo Uamuzi wa hukumu hiyo ni wa mwisho, hauna rufaa na ni wa lazima
#KenyaDecides2022 #Democracy
#Jamii Forums