Huyu Hapa Mwanamke Aliyefariki Akimkimbiza Mumewe Aliyekuwa na Mchepuko Kwenye Gari


MWANAMKE mmoja kutoka nchini Nigeria amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari wakati akimfukuzia mumewe aliyekuwa na mwanamke mwingine kwenye gari hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shuhuda wa tukio hilo, mwanamke huyo alimuona mume wake huyo akitoka kwenye saluni ya kike na mwanamke huyo anayedaiwa kuwa ni mchepuko wa mwanaume huyo ambapo mara baada ya kuwaona, mwanamkehuyo alikimbia na kuingia kwenye gari lake na kisha kuliondoa kwa kasi akiwa na lengo la kuwahi ili akasimame mbele yao na kuwazuia kupita, jambo ambalo halikufanikiwa na hivyo kujikuta akipata ajali mbaya.


Ajali iliyopelekea kifo Cha Mwanamke huyo
Mara baada ya ajali hiyo kutokea, mwanaume huyo alisimamisha gari lake na kisha kumshusha mwanamke aliyekuwa naye na baada ya hapo ndipo alikwenda kumsaidia mke wake ambaye alikimbizwa hospitali baada ya kuokolewa, mwanamke huyo alipoteza maisha baadaye akiwa hospitalini akipatiwa matibabu Zaidi kufuatia ajali aliyoipata.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad