Jinsi Mvenezuela 'alivyomfanya' Ruto kuwa Rais mteule, Julie Soweto





Raia wa Venezuela Jose Camargo ndiye aliyeamua kuwa Rais wa Kenya atakuwa nani, wakili Julie Soweto ameiambia Mahakama ya Upeo.

Mnamo Ijumaa, Wakili Soweto aliionyesha mahakama jinsi upangaji wa matokeo ulivyokuwa ukifanyika katika tovuti ya IEBC.

“Wewe ni mjuzi wa teknolojia na unaweza kufikia tovuti ya IEBC. Ninaomba twende kwenye tovuti ya fomu,” alisema.


Katika kaunti ya Murang’a, katika shule ya Msingi ya Gacharaigu, Soweto ilionyesha mahakama jinsi Camargo alivyofanya ujanja kwenye seva.

Mgeni huyo alikuwa mmoja wa raia wa Venezuela waliokamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kwa tuhuma za kuingilia mchakato wa uchaguzi.

Soweto alifanya wasilisho la video ya moja kwa moj ili kuonyesha hitilafu kutoka kwa tovuti ya umma ya IEBC.

Jina "Jose Camargo" lilikuwa upande wa kushoto wa fomu.



“Huyu mtu ndiye alikuwa anaingilia matokeo. Hii ni tarehe 9 Agosti na tuliambiwa hawakuwepo,” alisema.

"Tuliambiwa na Gumbo hakukuwa na wageni katika uchaguzi huu. Tuliambiwa hawakupata seva. Katika kona ya juu kushoto tuna jina la Jose Camargo."

Alisema fomu hizo zilinaswa na kutoa fursa ya mhusika kuamua ni zipi ambazo wangeweza kuzibadilisha kabla ya kuzituma kwenye tovuti.

"Fomu asili ya 34 A ni ya rangi ambayo ilipaswa kuonekana katika kituo cha kujumlisha kura," Alisema.

Soweto ilionyesha zaidi jinsi kifaa kimoja cha KIEMS kilivyosambaza matokeo kutoka maeneo tofauti.

"Je, kifaa kimoja cha KIEMS kinawezaje kusambaza kutoka maeneo mawili tofauti; Mlima Elgon na Nyeri?... Kwa sababu ya muda siwezi kuonyesha maelfu ya fomu ambazo tumetambua na suala moja," alisema.

Kabla ya Soweto kuja kusimama, Wakili Paul Mwangi alisema Camargo aliacha alama za vidole kwenye fomu hizo.

“Tunaamini kuwa hizi ni alama za vidole vya mmoja wa washukiwa wa wizi wa uchaguzi huu,” Mwangi alisema alipokuwa akionyesha korti fomu 34A kutoka Shule ya Msingi ya Gacharaigu.

Utafsiri: Samuel Maina

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad