Kajala na Harmonize hawana habari na tozo, wanakula bata hatarii



Kajala na Harmonize hawana habari na tozo, wanakula bata hatarii

Maisha wanayoishi mastaa Kajala Masanja na Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ni kama vile sio Wabongo, wanaishi kama mbele vile.

Suala la kwenda mapumzikoni katika mbuga za wanyama kwa ajili ya kupumzisha akili sio mpaka waandikiwe na daktari, wanafanya hivyo mara kwa mara.

Safari hii, mnara umesoma Lake Manyara National ambapo wawili hao wanaonekana wakila bata kwenye swimming pool wakiwa wawili tu na mpiga picha wao maalum ambaye hakuonekana pichani.

Kajala kuna wakati alikuwa na kigauni cha uchokozi kabla hajabaki na kinguo maalum cha kuogelea ambacho kinaacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi.

Baadhi ya maoni kwenye picha hizo ambazo Kajala kaziposti kwenye ukurasa wake wa Instagram, wapo waliompongeza lakini wengine wakiuliza kama wao hawajaguswa na makali ya tozo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad