Kampuni ya Vodacom yapata hasara ya bilioni 103.8, watumiaji wa M Pesa wamepungua

Kampuni hiyo ya Mawasiliano ilipanga kukusanya Tsh. Trilioni 1.06 katika mwaka ulioisha March 2022 lakini kutokana na athari za Tozo imepoteza 9.8% ya mapato na kukusanya Tsh. Bilioni 956 ambayo ni pungufu ya matarajio.

Ripoti hiyo ya Vodacoma inaeleza kuwa tozo hizo ziliongeza gharama za wateja kufanya miamala kwa kutumia simu za mkononi, hivyo kusababisha zaidi ya wateja milioni 1.3 kuacha kutumia huduma za M-Pesa.

Kutokana na hali hiyo, huduma ya M-Pesa ambayo imekua namba moja kwa ukusanyaji mapato kwa Vodacom Tanzania, ilishuka kwa 7.6% ya kiasi kilichokusanywa na kampuni hiyo.

Serikali ilianzisha tozo za miamala Juni 2021 ili kutafuta fedha zaidi za ujenzi wa miradi, hata hivyo, utekelezaji wake umepata ukosoaji na kusababisha kushuka kwa miamala ya kifedha kwa njia ya simu huku watu wakitumia njia nyingine mbadala za kutuma na kupokea pesa.

Ripoti hiyo ya Vodacoma inaeleza kuwa tozo hizo ziliongeza gharama za wateja kufanya miamala kwa kutumia simu za mkononi, hivyo kusababisha zaidi ya wateja milioni 1.3 kuacha kutumia huduma za M-Pesa. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad