Kwenye interview yake aliyoifanya hivi karibuni na kituo cha ABC NEWS, Ye (Kanye West) anaamini mwanae wa kwanza, North West (09) atakuwa ni moja ya wasimamiaji wa familia na brands za wazazi wake, hivyo ilimbidi siku moja kukaa naye chini na kumsihi mambo mbali mbali ya kufanya na kutofanya huko mbeleni.
Ye amedai miongoni ya hayo mambo ni kumsihi, kutoruhusu mtu yeyote kuchukia brands za wazazi wake, Kuwalinda wadogo zake na kuilinda familia yake kiujumla, ameyaongea hayo kwake kwasababu anajua North ni miongoni mwa watu wa familia ambao watahakikisha, hakuna mtu ataiba brands ambazo wazazi wake wamezitengeneza kwa muda mrefu.
Wapo baadhi ya watu wameona ni mapema sana kwa mtoto wa miaka 9 kuhusiwa vitu kama hivyo, huku wengine wakiona Ye yuko sahihi.
Unahisi mwanao anapaswa kuhusiwa akiwa na umri gani, na ni vitu gani utamuhusia zaidi?😁