Watu sita wameuawa, katika shambulio lililolenga basi eneo la magharibi mwa Cameroon lenye machafuko, lililokumbwa na mzozo wa umwagaji damu kati ya watu wanaotaka kujitenga na watu wa Serikali wanaozungumza Kiingereza.
Waziri wa serikali ya Cameroon, Rene Emmanuel Sadi amesema shambulio dhidi ya basi hilo lilitekelezwa na kundi la “magaidi waliokuwa na silaha nzito eneo la Fako katika linalozungumza Kiingereza kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Amesema, “shambulio hilo la kigaidi la kikatili na la kinyama lilisababisha vifo vya watu sita, akiwemo mwanamke mmoja na wanaume watano pamoja na wanane kujeruhiwa.”
Watu wanaozungumza Kifaransa wanaodaiwa kujitenga, wameshambulia basi na kuwauwa watu sita. Picha na VOA.
Sadi ameongeza kuwa, “Serikali ya Jamhuri ya watu wa Cameroon inalaani vikali shambulio hili la woga na la kuchukiza linalofanywa dhidi ya raia wasio na hatia.”
Mikoa ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi nchini humo, imekumbwa na mzozo wa umwagaji damu kati ya wanaotaka kujitenga kwa lugha ya Kiingereza na serikali kwa miaka mitano sasa.
Wazungumzaji wa Kiingereza, wanaunda idadi kubwa ya wakazi wa mikoa hiyo wakati Wacameroon wakizungumza Kifaransa na inaarifiwa Rais Paul Biya ameitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma tangu 1982.